Thursday, August 1, 2024

Blog ya"Oscar Health Inputs" inakukaribisha uweze kujifunza na kufahamu juu ya ugonjwa wa HOMA ya INI (HEPATITIS)

      UGONJWA WA HOMA YA INI NA MAMBO MUHIMU YA TUPASAYO KUFAMU.

                                                         INI ni nini ??



   INI  ni kiungo muhimu sana katika miili yetu, hufanya kazi nyingi sana zaidi ya kazi 500; Moja ya kazi kubwa ya Ini katika miili yetu ni Kuchuja na Kuondoa Sumu kutoka kwenye Damu.

kutokana na sababu mbalimbali zinzo sababisha miili yetu kukusanya sumu katika damu kama vile, UNYWAJI WA POMBE KUPITA KIASI, SUMU KWENYE DAMU,Au MAAMBUKIZI; husababisha ini hupata shida na kuvimba: hivyo INI hushindwa kufanya  kazi za kila siku katika miili yetu.

hii hali huitwa HOMA YA INI au HEPATITIS.


                                            VIRUSI WA HOMA YA INI NI WEPI??

Katika Bara letu la Afrika, maambukizi ya ya virusi wa homa ya ini ndio sababu kuu ya shida kwenye INI. Virusi vya homa ya Ini vipo  vya aina 5 ( A,B,C,D,E.)

Aina mbili za virusi ( B na C) ndio sababu kuu ya ugonjwa wa INI na husambaa kwa njia mbili, ambazo ni Damu na Maji maji ya mwilini, kama vile jasho, shahawa,mate na mengineyo.

virus aina B  huambukizwa kwa kupitia damu kutoka kwa mtu mwenye maambukizi ya virusi vya homa ya ini kundi B kwenda kwa mtu ambaye hana maambukizi,. hii yaweza kuwa ni kwa kuchangiwa damu iliyo kuwa haijapimwa kikamilifu vimelea vya homa ya INI, au kuchangia vitu vyenye ncha kali kutoka kwa mtu aliye ambukizwa kwenda kwa mtu asiye na maambukizi.

Virus aina C huambukizwa kwa kupitia mgusano wa majimaji ya mwili kutoka kwa mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa wa homa ya INI kwenda kwa mtu asiye na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya INI.


    DALILI KWA MTU MWENYE UGONJWA WA HOMA YA INI.

Dalili za mu mwenye maambukizi ya ugonjwa wa HOMA YA INI zimegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni  ( dalili za muda mfupi- ACUTE HEPATITIS) na Dalili za KUDUMU ( CHRONIC HEPATITIS)

Dalili hizi za mwanzo huanza kutokea ndani ya miezi 6 baada ya mtu kuambukizwa virusi vya homa ya INI. Hata hivyo dalili hhizi huweza kutokea kwa baadhi ya watu na sio kwa kila mtu. hivyo uonapo dalili hizi tafadhari fika kituo cha kutolea huduma kilicho karibu nawe.

        1.kupoteza hamu ya kula

       2. kichefuchefu na kutapika

       3. mwili kuuma

       4. mkojo kuwa na rangi iliyo kolea kama Coca - Cola

       5. kupata manjano kwenye macho, viganja vya mikono/ kucha au mwili mzima.

        6. kuvimba tumbo na kupumua kwa shida.


Dalili za kudumu: ( Chronic Hepatitis) - watu wenye maambukizi ya kudumu ya virusi vya homa ya ini, mara nyingi huwa hawana dalili. kadri muda unavyo enda virusi husababisha INI kusinyaa(CIRRHOSIS) na kushindwa kabisa kufanya kazi vyema.

Pia maambukizi ya virusi vya Homa ya INI huchangia kupata SARATANI YA INI.


        MAKUNDI YALIYO KATIKA HALI HATARISHI KUPATA MAAMBUKIZI YA HOMA YA INI.

Haya ndio makundi ya watu walio katika nafasi kubwa sana ya mkuweza kupata maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa INI.

  • watoto wote 

  • watu wote wanao tumia dawa za kulevya na kujidunga.
  • watu wote ndani ya familia wanao ishi na mtu mwenye virusi vya homa ya INI.
  • watu wote wanao fanya biashara ya ngono.
  • watu wote wanao kunywa pombe kupitiliza.
  • watu wenye wapenzi wengi
  • watumishi wote wa idara ya afya

   JE, NI MUHIMU KUPIMA  ILI KUJUA KAMA NINA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UGONJWA  WA HOMA YA INI ??

watu wengi huishi na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa homa ya INI bila kufahamu.
kwa kawaida katika kipindi fulani cha maisha mtu 1 kati ya 3 huambukizwa virusi vya HOMA YA INI. Baada ya kuambukizwa kuna kundi la watu hubaki na maambukizi ya kudumu ya virusi vya homa ya INI ambayo huwa hayana Dalili yoyote na kuendelea kuua INI kimya kimya.

Dalili huja kuonekena waziwazi miaka mingi baada ya mtu kuwa ameambukizwa virusi hivyo vya homa ya INI. Huonekana wakati tayari INI limenyauka au lina kansa.

Hivyo mtu aliye na maambukizi ya virusi vya homa ya Ini aina B akianza matibabu mapema, anaweza kuzuia INI lake lisiharibike sana. Pia kwa mwenye maambukizi ya virusi vya homa ya INI aina C matibabu ya dawa  wiki 12 husaidia kumaliza virusi vyote.

     kwa tafsiri ya athari hizi za virusi hawa wa ugonjwa wa homa ya Ini ni lazima na ni muhimu sana kwa kila mtu kuweza kupima Virusi vya ugonjwa huu wa Homa ya INI kabla ya athari kuanza kujitokeza.



        NINI KIFANYIKE KUJIKINGA NA VIRUSI VYA HOMA YA INI.

Ugonjwa wa homa ya Ini una weza kukingwa na kukufanya upunguze hatari ya kuweza kuambukizwa.

ili kuweza kujikinga ni lazima uweze kuepuka vitu vyote vinavyo weza kukupelekea kuambukizwa virusi vya homa ya Ini.

vile vile unatakiwa kuweza kupimwa maambukizi ya virusi vya homa ya Ini katika vituo vyetu vya kutolea huduma za afya, na kuweza kupatiwa matibabu kama utakutwa na maambukizi na kupatiwa chanjo kama utakutwa hauna maambukizi.

mzazi ni lazima uweze kuhakikisha mtoto wako anapata chanjo kwa wakati na kufuata ratiba yake ya chanjo.

            chanjo hutolewa kwa njia ya sindano katika awamu 3 tofauti.

  1. Chanjo ya kwanza pale tu,  unapo pima na kukuta hauna maambukizi ya Virusi vya Homa ya Ini.
  2. sindano ya pili hutolewa baada ya mwezi mmoja tangu ulipo choma chanjo ya kwanza.
  3. sindano ya tatu baada ya miezi sita tangu ulipo choma chanjo ya kwanza.



        JE VIRUSI VYA UGONJWA WA HOMA YA INI VINAWEZA ISHI NJE YA MWILI??

Tafiti zinaonyesha virusi vya Ugonjwa wa Homa ya Ini vinaweza kuishi nje ya mwili kwa muda wa siku 7, bado vikiwa na uwezo wa kuambukiza mtu mwingine.

tafiti pia zina onyesha hata damu iliyo kauka yenye virusi vya Homa ya Ini huwa na uwezo wa kuambukiza.

3 comments:

  1. Asante kwa elimu hii Daktari, nikitaka chanjo utaratibu upoje?

    ReplyDelete
    Replies
    1. chanjo zina patikana vituo vyote vya kutolea huduma za afya TANZANIA

      Delete
  2. Umetisha sana Jamaa Keep it content ni Nzuri, zinaeleweka kwa kila mtu

    ReplyDelete