Tuesday, August 27, 2024

FAHAMU MPANGO BINAFSI WA MAMA MJAMZITO KUJIFUNGUA SALAMA

MPANGO BINAFSI WA MAMA MJAMZITO WA KUJIFUNGUA





ANDAA,ZUNGUMZA NA MWENZI WAKO,JAZA MPANGO



  • Fahamu tarehe ya kujifungua.
  • Fahamu na uhakikishe kituo cha kutolea huduma za afya au hospitali utakapojifungulia.



  • Fanya mpango wa usafiri wa kukufikisha mapema kwenye kituo cha kutolea huduma za afya utakapojifungulia.
  • Nani atakaye kusindikiza kwenye kituo cha kutolea huduma za afya mapema ili ujifungulie huko.
  • Tayarisha mfuko utakapoweka nguo za mtoto na mahitaji yote wakati ukiwa katika kituo cha kutolea huduma za afya.
  • Nani utakayemwachia nyumba utakapoenda kujifungua?
  •  Jadili na mwenza wako na mtoa huduma iwapo unataka kubadili mpango.


UFIKAPO KATIKA KITUO CHA KUTOLEA HUDUMA HIVI NDIVYO VIPIMO MUHIMU UNAVYO TAKIWA KUPIMWA MAMA MJAMZITO.

  • Kipimo cha presha ya damu
  • Kipimo cha kiwango cha damu
  • Kipimo cha mkojo
  • Mtoto anavyoendelea kukua tumboni
  • Vipimo vinavyofanyika angalau mara moja wakati wa ujauzito
  • Kipimo cha kundi la damu
  • Kipimo cha magonjwa ya zinaa mfano Kaswende
  • Kipimo cha Virusi Vya Ukimwi kwako na mwenza wako(kawaida mara mbili)
  • Hakikisha unapata vitu hivi
  • Chandarua chenye dawa( viatilifu)
  • Chanjo za pepopunda
  • Vidonge vya kuongeza damu(Tumia kila siku wakati wa ujauzito na endelea kutumia vidonge vya kuongeza damu mpaka miezi mitatu baada ya kujifungua)
  • Dawa za minyoo(Tumia mara moja baada ya miezi mitatu ya ujauzito
  • Vidonge vya SP kuanzia wiki ya 14 ya ujauzito na kila unapohudhuria kituo cha kutolea huduma za afya.

DALILI ZA HATARI KABLA YA KUJIFUNGUA/WAKATI WA KUJIFUNGUA/BAADA YA KUJIFUNGUA

Uonapo dalili hizi nenda kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu nawe mara moja!!!

  • Kutoka damu ukeni
  • Kuumwa sana na kichwa na kuona maluweluwe/kushindwa kuona
  • Kupoteza fahamu au mtukutiko mwili/kifafa cha mimba
  • Kuchoka haraka ,kupumua kwa shida
  • Homa
  • Mtoto kuacha au kupunguza kucheza tumboni.
  • Dalili za ishara za uchungu wa kujifungua
  • Mkazo na kuachia kwa misuli ya mfuko wa uzazi unaoendelea kuongezeka na kusababisha  maumivu makali ya tumbo na kiuno hadi kujifungua.
  • Kutokwa mchozo ute wenye damu.

KUMBUKA: Kama unaishi mbali na kituo cha kutolea huduma za afya ,ni busara kuhamia kwa muda karibu na kituo hicho,kadiri siku ya kujifungua inavyokaribia.


imeandaliwa na : oscar kilengule

mawasiliano: 

email: aronkilengule@gmail.com

whatsaap: +255758420006

calls: +255677706007


Thursday, August 22, 2024

zijue faida na umuhimu wa vyakula vinavyo ongeza maziwa mama anaye nyonyesha

LISHE YENYE FAIDA KWA MAMA ANAYE NYONYESHA NA MTOTO WAKE.



 Kwa nini kunyonyesha kunanifanya niwe na njaa sana?



Licha ya hadithi ya kula kwa ajili ya watu wawili wakati wa ujauzito, kalori 200 tu za kwa siku nyinginezo katika hitaji la ziada la kumaliza ujauzito. Linganisha hii na makadirio ya kalori 330 kwa siku zinazotumiwa wakati wa kunyonyesha - hiyo ni sawa na kukimbia maili kadhaa! Ingawa mwili wa mama mpya unaweza kutumia akiba katika mafuta yaliyowekwa wakati wa ujauzito, kula kidogo zaidi kusaidia kusaidia kusaidia uzito wa mtoto, lakini ni bora usawa wa afya wa vyakula virutubishi vingi. .Wakati uchovu na kunyimwa usingizi huanza, kula vizuri ni moja ya mambo ambayo yataweza kumaliza kumaliza.

Kula afya kwa mama wanaonyonyesha

mboga za matunda


Milo ya msingi juu ya viazi, mkate, wali, pasta au wanga nyingine ya wanga

Kuwa na bidhaa mbadala za maziwa au maziwa (kama vile vinywaji vya soya na mtindi)

 mafuta ya chakula, na kula kwa kiasi kidogo

Kula vyakula vyenye mafuta mengi, chumvi na sukari mara chache na kwa kiasi kidogo

Ushauri wa jumla wa kula kiafya, kulingana na Mwongozo wa Eatwell, ni mahali pazuri pa kuanza kupanga kwani hii kushughulikia kuwa unapata mchango muhimu kwa mwili wako. Kupata virutubish vya kutosha kutatumika hadi kusaidia kwamba maziwa ya mtoto yanatunzwa vizuri zaidi, hivyo akina mama wanaonyonyesha wanahitaji kulinda wanajaza matumizi hivyo.

Kunywa maji ya kutosha

Kupata maji ya kutosha ni muhimu sana wakati wa kunyonyesha kwani huhakikisha ugavi mzuri wa maziwa. Akina mama wengi wanaona kwamba kunyonyesha kunawafanya wao na kiu, na upungufu wa maji mwilini hupoteza nguvu nyingi, kwa hiyo kunywa kinywaji kila wakati unapoketi ni jambo zuri.

Maji pengine ni chaguo rahisi na bora zaidi, lakini maziwa yenye mafuta kidogo na hata chai isiyo na sukari au kahawa (kuwa makini na kiasi cha kafeini uliyo nayo) zote ni chaguo nzuri.

Usisahau kuwa na maji karibu na kitanda kwa ajili ya kunywa usiku.

ik

Vitafunio rahisi

ya akina mama wanaona kwamba wana hamu ya kula, hivyo hakikisha kwamba vitafunio vingine afya viko karibu. Matunda, matunda yaliyokaushwa (kama parachichi, tini na prunes), nafaka ya kinywaa kinywa na maziwa, toast au oatcakes zote ni bora na za haraka. Hakuna haja ya kununua gharama za gharama kubwa wakati wa kunyonyesha, lakini ongeza vitamini D.

Je, nijiepushe na vyakula vyovyote wakati wa kunyonyesha?

Habari njema ni kwamba vyakula vingi havikuwa na kikomo wakati wa ujauzito kwenye ujauzito tena - kwa hivyo pâté na jibini la bluu vimerudishwa menyu. Hakuna vyakula vilivyozuiliwa kabisa wakati wa kunyonyesha, lakini baadhi huja tahadhari.

Pombe Licha ya ushauri kutoka kwa baadhi ya watu itaongeza maziwa, cha kusikitisha chupa ya stout haiwezi kutekeleza utoaji wa maziwa, na ushahidi fulani unaoonyesha kunywa mara kwa mara zaidi ya vitengo viwili vya pombe kila siku kutekeleza kuathiri ukuaji wa mtoto.

Hata hivyo, mara kwa mara kunywa pombe hakuna kitu ambacho kinaweza kutumika katika chochote, hivyo usijali kuhusu kuwa na glasi isiyo ya kawaida ya divai. Pombe inapoingia kwenye maziwa ya mama na kuathiri ladha na harufu yake, ulishaji wa mtoto unaweza kuathirika. Epuka hili kwa kulisha saa mbili hadi tatu baada ya kunywa pombe au kukamua maziwa kabla ya kunywa pombe.

ik

Chanzo cha picha,Picha za Getty

Maelezo ya picha,kula vizuri wakati wa ujauzito na kunyonyesha pia

Kafeini Wakati wa kunyonyesha, ni bora kafeini hadi 200mg kwa siku. Mug ya chai ina karibu 75mg, kahawa ya chujio 140mg na kopo la cola (pamoja na chakula) 40mg. Kafeini hupita ndani ya maziwa ya mama na, ingawa haina madhara, inaweza kuwa baadhi ya baadhi ya watoto wasitulie, kwa hiyo inaweza kutumika kubadili njia zisizo na kafeini.

Samaki Watu wazima wote kusimama kula karibu sehemu mbili za samaki kila wiki. Samaki wenye mafuta ni wa ajabu kwa kutoa mafuta ya omega-3, ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto, lakini wakati wa kunyonyesha, lengo la samaki ya mafuta si zaidi ya sehemu mbili kwa wiki, kama vile makrill, lax na dagaa.

Pengine hakuna mtu kwamba papa ni sehemu kubwa ya mlo wako wa kila, lakini NHS i kuweka uepuke papa, marlin na swordfish kwa kuwa unaweza kuwa na zebaki nyingi na uchafu mwingine - ikiwa huwezi kupinga samaki kabisa basi sikukuu zaidi ya mara moja kwa wiki.

Kuondoa baadhi ya baadhi ya mitishamba kama vile fenugreek inaripotiwa kusaidia utoaji wa, mingine kama iliki inadhaniwa kuacha maziwa. Kwa kweli, kuna ushahidi mdogo kwa aidha, hivyo kutumia mimea ya upishi ni sawa. Viungo pia ni salama, ingawa ninaweza kuhamisha ladha kwa maziwa, na kuwafanya watoto wengine kuwa na wasiwasi.

Baadhi ya vyakula, kama vile kabichi, maharagwe na chipukizi zaidi kuathiri wengine wa mtoto, na kuwafanya wao na gesi na wasistarehe. Ikiwa unafurahia kula vyakula hivi, ni sawa, lakini jaribu kuvizuia kwa siku kadhaa ikiwa vinaonekana kuzua gesi kwa mtoto. Kwa ujumla, hakuna ushahidi kwamba chakula cha mama gesi kwa watoto wanaonyonyesha.

Hatimaye, karanga, ikiwa ni pamoja na siagi ya karanga, ni salama kuliwa na haitamfanya mtoto awe katika hatari kubwa ya kupata mapato ya karanga. Siagi ya karanga kwenye keki za oatcakes ni vitafunio vingi vya lishe na kuongeza nishati!


imeandaliwa na: oscar kilengule

email: aronkilengule@gmail.com

whatsaap: +255758420006

calls :+255677706007


Wednesday, August 21, 2024

ZIJUE DALILI, SABABU NA KINGA DHIDI YA MIMBA KUHARIBIKA

Chanzo Cha mimba Kuharibika

Mimba kuharibika mara kwa mara
Mimba kuharibika au miscarriage ni kitendo cha kupoteza kichanga kwa mama mjamzito kabla ya muda wa kujifungua kuwadia. Mara nyingi hutokea ndani ya miezi mitatu ya mwanzo baada ya kushika ujauzito. sababu za  mimba kutoka zinatofautiana kwa kila mwanamke. Zifuatazo ni dalili kwamba mimba yako imeharibika

Dalili za Mimba Kuharibika.

Kwa kutegemea na hatua ya ujauzito wako, dalili hutofautiana . Wakati mwingine hujitokeza haraka pengine kabla hujajua kama una ujauzito tayari mimba inakuwa imeharibika. Dalili hizi ni pamoja na

  • maumivu ya mgongo
  • kuvuja damu ukeni
  • kutoka kwa tishu za mabongemabonge katika uke
  • misuli kukaza na
  • maumivu makali ya tumbo

Hakikisha unaongea na daktari haraka iwezekanavyo unapoanza kuona dalili kama hizi. Kumbuka inawezekana kabisa kupata dalili hizi lakini mimba yako ikawa salama. Lakini ni muhimu kwa dactari kujiridhisha kama uko salama.

Namna 5 za Mimba Kuharibika na Kutoka.

Kuna aina namna nyingi za mimba kuharibika. Kwa Kutegemeana na sababu ya mimba yako kutoka mapema pamoja na hatua ya ukuaji wa mimba aina hizi zinaweza kuainishwa kama ifuatavyo

  • Blighted ovum: ni pale yai lililorutubishwa linajipandikiza kwenye ukuta wa uterus lakini mimba haikui na kupelekea kuharibika.





  • Complete abortion: ni pale kiumbe kilichotungwa kinatolewa nje ya mfuko wa mimba. Inaweza kusababisha damu kuvuja



  • Missed abortion: Ni pale kiumbe kidogo kufariki tumboni pasipo kutoa viashiria vyovyote
  • Reccurent abortion: ni pale mimba zako zinapotoka mfululizo mara 3 au zaidi ndani ya miezi mitatu ya kwanza
  • Ectopic miscarriage: Mimba kujishikiza mahali pengine hasa kwenye mirija ya uzazi badala ya mji wa mimba na kupelekea kutoka kwa mimba
  • Threatened abortion: Ni pale mjamzito anaanza kupata dalili za kutokwa na damu ukeni na maumivu yanayoashiria kuharibika kwa mimba. 

Nini hasa Kinasababisha Mimba Kuharibika Na Kutoka Kabla ya Wakati?

Wakati wa ujauzito mwili hupeleka virutubisho na homoni kwenye kiumbe kinachokua. Hivi vyote husaidia kiumbe kuwa na afya njema na kukua vizuri. Mimba nyingi zinazoharibika ndani ya miezi mitatu ya kwanza ni kutokana na kiumbe kudumaa. Kuna sababu nyingi zinapelekea Mimba kuharibika mapema kama ifuatavyo.

Vinasaba

Karibu 50% ya mimba zinazotoka kabla ya wakati ni kutokana na makosa kwenye vinasaba. Makosa yanaweza kufanyika pale seli za kiumbe zinapogawanyika. au inaweza kutokana na majeraha kwenye mbegu ya kiume au yai la mwanamke.

Matatizo ya Kiafya

Matatizo ya kiafya pamoja na mtindo wa maisha unaweza kuletekeza mimba kutoka, hasa kwenye kipindi cha miezi mitatu ya pili (second trimester). Kumbuka mazoezi ya mwili na kushiriki ngono haiwezi kusababisha mimba kutoka. Mazingira yafuatayo yanaweza kuhataraisha mimba yako

  • lishe mbaya inayokosa virutubisho  vingi
  • matumizi ya pombe, madawa na sigara
  • matatizo kwenye tezi ya thairodi ambayo hayajatibiwa
  • maambukizi kwenye njia ya uzazi
  • msongo wa mawazo
  • uzito mkubwa na kitambi
  • matatizo kwenye mlango wa kizazi (cervical incompetence)
  • kulegea kwa mfuko wa mimba
  • shinikizo la damu kuwa juu zaidi
  • kutumia chakula chenye sumu na
  • matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari

Jinsi gani unaweza Kuzuia Mimba Kuharibika??

Kwa kiasi kikubwa mimba kuharibika inaweza kuepushwa japo siyo kila mazingira mfano kama tatizo limetokana na vinasaba. Zifuatazo ni sheria za kiafya za kuzuingatia ili kupunguza hatari ya mimba kutoka.

  • Usitumie pombe, madawa, na kuvuta sigara wakati wa ujauzito
  • Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara ili kuimarisha ukuaji wa kichanga tumboni
  • Jikinge na maambukizi kwenye njia ya uzazi kwa kunawa mikono kwa maji safi na kutoambatana na watu wanaoumwa
  • Usianye kazi ngumu wala kubeba vitu vizito ukiwa na mimba
  • Endapo ni mimba nyingi zimeshaharbika, kwa miezi minne ya mwanzo usifanye ngono kabisa
  • Usipate bodaboda au chombo cha usafiri kinachokurusharusha ni hatari kwa mimba yako
  • Usitumie vyakula na vinywaji vyenye caffeine kama kahawa wakati wa ujauzito
  • Kula mlo mzuri wa vitamin ili kuimarisha ukuaji wa kichanga na
  • Usitumie dawa yoyote kama hujapewa hospitali

Nini cha kufanya pale Ujauzito Unapoharibika na Kutoka.

Baaada ya mimba kutoka mwili huanza kurudi katika hali ya kawaida taratibu taratibu. Kuimarika haraka kwa mwili kunategemea mimba yako ilikuwa na umri gani kabla haijatoka. Baada ya mimba kutoka unaweza kupata dalili hizi

  • Kutokwa na damu ukeni kama damu ya hedhi
  • Maumivu ya tumbo na
  • Kuvimba kwa matiti

Mwili utaanza kupata tena hedhi baada ya week 3 mpaka 6 baada ya mimba kutoka. Ni vizuri kujipa mda wa kupumzisha mwili na ukapata usaidizi wa kifikra na hisia ili kuondokana na msongo wa mawazo.

 Ni upi muda sahihi wa kubeba Mimba tena Baada ya Mimba ya Awali Kuharibika.

Kabla hujaamua kushika ujauzito mwingine ni vizuri kuhakikisha mwili uko sawa na afya yako ni njema. Ukiwa na afya njema inapukupunguzia hatari ya mimba nyingine kuharibika.

Daktari hufanya vipimo kadhaa ili kujua chanzo cha tatizo lako; Vipimo hivi vinajumuisha

  • Vipimo vya damu kuangalia kama una mvurugiko wa homoni
  • Kupima vinasaba
  • Kipimo cha mkojo 
  • Kipimo cha utrasound

Unashauriwa kujipa mda wa kupumzika walau miezi 8 mpaka mwaka mmoja kabla hujaamua kushika ujauzito tena.

Uonapo mama aliye kuwa mjamzito ana onyesha dalili hizi, tafadhari mpeleke haraka kituo cha afya kilicho kaaribu nawe ili kuepusha madhara makubwa yatokanayo na mimba kuharibika.

Kama umependa makala yetu hii basi usisite kutuandikia maoni yako.

imeandaliwa na kuhaririwa na: oscar aron kilengule

mawasiliano:

email: aronkilengule@gmail.com

whatsaap +255758420006

calls: +255677706007

Monday, August 19, 2024

JE WAZIJUA VEMA ATHARI NA DALILI MBAYA KWA MAMA MJAMZITO ???.



Kipindi cha ujauzito kinaambatana na mabadiliko mengi sana ya mwili, pamoja na mabadiliko ya kimaisha pia kwenye kujiandaa kumpokea mwanafamilia mpya. 

Ni kipindi pia ambacho waweza kuwa na hofu sana kuhusu mimba yako, na utakuwa mwangalifu sana. Hapa chini ni maelezo a kina juu ya dalili mbaya kwa mjamzito na hatua za kuchukua mapema.

Mabadiliko mengi ambayo utayaona mwilini mwako, jua kwamba ni kawaida na ni lazima uyapitie. Dalili nyingi mfano kuumwa nyonga, tumbo kuunguruma, kukosa choo, kizunguzungu nk zinakuja na kupotea.

mama mjamzito kuwa huru kujieleza kwa mtoa huduma dalili zote za hatari, maana ni lazima ata tunza siri ya yale mliyo yazungumza.

mtoa huduma za afya akimthibitishia mteja kuwa hato toa siri za mazungumzo yao.


Je dalili mbaya zinaisha mapema?

Baadhi ya dalili waweza kukaa nazo mpaka siku unajifungua, na kuna zingine zinakuja na kupotea. Hapo ndipo yatakiwa kuwa makini kwa kila dalili unazopata. Kuna dalili zingine hatari ambazo haitakiwi upitishe hata siku 1 bila kwenda hospital, endapo utaziona.

Dalili za Kawaida Ambazo siyo hatarishi

Dalili nyingi kati ya hizi siyo hatari, na haitakiwi kupata hofu sana. Japo unaruhusiwa kumpigia daktari wako na kumuuliza ili upate uhakika zaidi. Dalili nyingi ya hizi zinajitokeza mimba ikiwa changa, na zingine baadae

  • kutapika
  • kutokwa na uchafu mwingi ukeni
  • kichwa kuuma
  • uchofu na kizunguzungu
  • maumivu yanayokuja kwa haraka na kupotea
  • kupungua uzito
  • kuhisi joto kali
  • kushindwa kuvuta hewa vizuri
  • mawazo, na kupata hofu ana kushindwa kufanya kazi zako vizuri

Dalili mbaya kwa mjamzito.

Dalili hizi zinatokea mda wowote wa ujauzito. Japo mimba inapokuwa changa zaidi ndipo hatari ya mimba kuharibika inakuwa kubwa, ila watakiwa kuwa makini kipindi chote.

Dalili hatarishi ni pamoja na

1.Kutokwa na damu/ Bleed ukiwa mjamzito



Kitendo cha kutokwa damu/bleed ukiwa na mimba siyo ishara nzuri hata kidogo, ni kiashiria kwamba kuna tatizo. ikiwa unatokwa damu nzito, na una maumivu makali ya tumbo upande wa kushoto au kulia na unajihisi kuishiwa nguvu, hii inaweza kuashiria mimba imetunga nje ya kizazi.

Mimba ikitunga nje ya kiazi haiwezi kukua, inatakiwa kuondolewa ma[pema kwa upasuaji. Mimba hiozi huitwa ecopic, endapo haitaondolewa mapema, mgonjwa anaweza kupoteza maisha.

Kama damu zinatoka nzito, tumbo linauma kuzunguka kitovu, hii inaashiria mimba imeharbika, na hii inatokea zaidi mimba ikiwa chini ya wiki 12. Sisemi kwamba mimba kubwa kubwa haziharbiki, hapana. Ni kwamba mimba nyingi zinaharbika zikiwa changa.

2.Kutapika na kichefuchefu kupita kiasi



Kwa mjamzito ni kawaida kupata kichefuchefu, lakini kama tatizo ni kubwa inaweza kuashiria shida kubwa ya kiafya. Kama unashindwa mpaka kula au kunywa chochote, hapo utaishiwa maji. Na kuishiwa maji inaweza kuhatarisha ujauzito wako.

Kama unahisi kizunguzungu kinakutesa sana, ongea na daktari atakupa dawa ya kupunguza makali yake.

3.Mtoto kuacha kucheza

Mtoto kupunguza kucheza inaweza kuashiria kachoka, hii ni kawaida isikupe hofu. ila kama hachezi kabisa kwa siku nzima, hapo kuna shida kubwa.

Sasa ili kugundua tatizo, inashauriwa ukiona mtoto hachezi mda mefu, jaribu unywe kitu cha baridi. Kisha lala kwa ubavu, na fatilia kama mtoto ataanza kucheza.

Mpigie daktari, ama nenda hospital haraka endapo utagundua mtoto ameacha kucheza. Daktari atafanya vipimo kuona kama kuna hatari yoyote.

4.Kupata uchungu mapema mimba ya miezi 7



Kupata uchungu na mimba haijatimiza umri wa kujifungua, ni dalili mbaya. Kama tumbo linavuta na kuachia na hii hali itokee mara chache na kuisha hilo ni kawaida. Kwani hata ukifika kileleni baada ya tendo, lazima utahisi tumbo kuvuta.

Lakini endapo tumbo linavuta na kuachia, kisha baada ya dakika 10 linaanza tena kuvuta na kuachia, hiyo ni ishara ya kuelekea kuzaa njiti. wahi kituo cha tiba kilicho karibu yako kwa msaada zaidi.

5.Chupa kupasuka mapema ni dalili mbaya kwa mjamzito

Tunaposema chupa, tunamaanisha ule mfuko unaobeba mtoto. Mfuko huu unakuwa na maji yanayomlinda mtoto asiumie. Mfuko unapasuka pale mama akianza uchungu na yupo tayari kujifungua. Endapo mfuko utapasuka mapema na mtoto akaendelea kubaki tumboni, mtoto atakosa hewa na kupoteza uhai.

Maji haya ni tofauti na mkojo, kwani hayaishi mapema yakianza kuvuja. Kwahivo tazama ukiona dalili ya kuvuja maji ukeni, tena maji mengi, nenda hospitali haraka.

6.Maumivu makali yasiyoisha kwenye kichwa, tumbo na kushindwa kuona vizuri

Hizi dalili zinaweza kuashiri kupanda kwa presha kitaalamu (preeclampsia) . Hili ni tatizo baya na linaweza kupelekea kifafa cha mimba. Tatizo linaambatana na dalili za presha kupanda na protini nyingi kwenye mkojo, hasa inatokea baada ya week 20 za ujauzito. Hakikisha unaenda hospital haraka endapo unahisi dalili hizo.

Nawezaje kujizuia nisipate dalili mbaya kwa ujauzito wangu?

Ukweli ni kwamba ni vigumu sana kujizuia asilimia zote kupata dalili mbaya kwenye ujauzito. Lakini kuna vitu vichache unaweza kufanya kupunguza hatari ya mimba kuharibika kabla ya muda wake.

Hudhuria clinic zote na upate dawa za kuongeza damu mapema kabisa. Unapoenda clinic mtoa huduma za afya atachukua historia yako na kukwambia endapo upo kwenye kundi hatarishi. Utapewa ushauri wa kina kuhusu lishe na afya ya akili.



Imeandikiwa na : oscar aron kilengule
Imehaririwa na Grace Kashegwe ( mratibu wa huduma za uzazi mama,baba na mtoto) halmashauri ya wilaya ya karagwe - kagera.

mawasiliano:
email: aronkilengule@gmail.com
whatsaap: +255758420006
calls: +255677706007